Ulimwengu kurudi Januari

Tuesday November 14 2017

 

By DORIS MALIYAGA

STRAIKA, Thomas Ulimwengu, amejificha katika nchi moja Ulaya akijifua kwa mazoezi binafsi ya uwanjani baada ya kuruhusiwa na daktari wake aliyemhakikishia ataanza kucheza mechi za ushindani Januari mwakani.

Ulimwengu ambaye anakipiga AFC Eskilstuna ya Sweden lakini kwa sasa hajaungana nao na amejificha katika nchi moja huko Ulaya akijifua ili awe sawa.

“Namshukuru Mungu naendelea vizuri, nimeanza kufanya mazoezi ya uwanjani ya kwangu binafsi, kwani awali nilikuwa nafanya ya viungo tu,” alisema Ulimwengu kwa njia ya simu.

“Hata hivyo sijajiunga na klabu yangu na sipo Sweden, kuna nchi nimejificha huku huku Ulaya najiweka sawa kwanza na daktari wangu ameniambia, nitarudi uwanjani kuanza kucheza Januari mwakani.”

Ulimwengu ambaye ni straika tegemeo wa Taifa Stars, alikaa nje ya uwanja baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini.

Anasema anaamini atakuwa sawa mapema.