Ujio wa Rais Magufuli washusha kiingilio Simba vs Kagera

Wednesday May 16 2018

 

Dar es Salaam. Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao amesema kiingilio kwa mechi ya Simba ambacho awali kilikuwa Sh3,000 sasa kimeshusha hadi Sh2,000.

Hatu hiyo imefikiwa  ili kuwapa nafasi mashabiki na wapenzi wa kalbu hiyo kwenda kushuhudia tukio la  klabu yao kukabidhi kombe lao la ubingwa msimu huu.

Awali, kulikuwa na minong’ono iwapo Rais angeweza kufika kwenye tukio hilo kubwa la kihistoria, hata hivyo TFF TFF wamethibitisha kuwepo kwake na kuondoka sintofahamu iliyokuwa imejitokeza.

Simba itakutana na Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ikiwa tayari imetawazwa kuwa bingwa baada ya Yanga kupoteza mchezo wake wiki iliyopita dhidi ya Tanzania Prisons.