Uhamisho wa Morata haijawahi tokea Hispania

Madrid, Hispania. Uhamisho wa Alvaro Morata kwenda Chelsea kwa gharama ya euro 80 milioni unamfanya kuwa mshambuliaji ghali zaidi katika historia ya wachezaji wa Hispania.

Uhamisho huo si tu nampa sifa hiyo, lakini unamfanya mshambuliaji huyo kuingia katika orodha ya wachezaji kumi ghali zaidi kwa sasa.

Katika orodha hiyo nafasi ya nane inashikiriwa na kocha ambaye anamuuza, Zinedine Zidane aliyejiunga na Real Madrid mwaka2001 kwa euros 75milioni.

Uhamisho ghali zaidi kwa sasa ni ule wa euro 105milioni waliotoa Manchester United kumnunua kiungo Paul Pogba kutoka Juventus mwaka 2016.

Dau la Mfaransa huyo lilivunja rekodi ya muda mrefu iliyowekwa na Cristiano Ronaldo aliyekuwa akiongoza tangu 2009, wakati aliponunuliwa kutoka Old Trafford na kuhamia Madrid kwa euros 96milioni pia Real ilitumia kiasi cha euros 91 milioni kumnasa Gareth Bale miaka minne iliyopita.

Mshambuliaji mwingine wa zamani wa Madrid anakamata nafasi ya nne, Gonzalo Higuain aliyehama kutoka Napoli kwenda Juventus kwa euro 90 milioni.

Barcelona ipo katika nafasi ya tano na sita katika oradha hiyo ikiwa na Neymar na Luis Suarez iliyowasajili kutoka Santos na Liverpool.

Morata pia anakuwa mchezaji ghali kuuzwa na Madrid, kwa kuwa uhamisho utaivunja rekodi ya euro 75milioni wakati walipouza Angel Di Maria kwa Manchester United mwaka 2014.

Orodha ya wachezaji ghali

1. Paul Pogba, 2016. Juventus kwenda Manchester United - euro105m.

2. Cristiano Ronaldo, 2009. Manchester United kwenda Real Madrid - euro96m.

3. Gareth Bale, 2013. Tottenham kwenda Real Madrid - euro 91m.

4. Gonzalo Higuain, 2016. Napoli kwenda Juventus - euro90m.

 5. Neymar, 2013. Santos kwenda Barcelona - 85m euros.

6. Romelu Lukaku, 2017. Everton kwenda Manchester United - euro85m.

7. Luis Suarez, 2014. Liverpool kwenda Barcelona - euro81m.

 8.   Alvaro Morata, 2017. Real Madrid kwenda Chelsea - euro80m.

9. Angel Di Maria, 2014. Real Madrid kwenda Manchester United euro 75m.

10. Zinedine Zidane, 2001. Juventus kwenda Real Madrid - 75m euros.

11.James Rodriguez, 2014. Monaco kwenda Real Madrid - euro 75m.

12. Kevin de Bruyne, 2015. Wolfsburg kwenda Manchester City - euro 74m.

13.  Zlatan Ibrahimovic, 2009. Inter kwenda Barcelona - euro69.5m.

14. Raheem Sterling, 2015. Liverpool kwenda Manchester City - euro68m.

15.  Kaka, 2008. Milan kwenda Real Madrid -  euro 65m.