Tshabalala: Hatuwaogopi Gor Mahia

Muktasari:

  • Simba na Gor Mahia zinakutana na pambano la fainali ya SportPesa Super Cup ambapo mshindi atazawadiwa Dola 30,000 (Sh68 milioni) pamoja na safari kwenda nchini England kucheza na Everton.

Nakuru. Nahodha wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala' amesema hawana woga wowote dhidi ya mabingwa wa Kenya, Gor Mahia na watapambana ili kushinda dhidi yao hapo kesho Jumapili.

Simba na Gor Mahia zinakutana na pambano la fainali ya SportPesa Super Cup ambapo mshindi atazawadiwa Dola 30,000 (Sh68 milioni) pamoja na safari kwenda nchini England kucheza na Everton.

Tshabalala alisema wachezaji wote wa Simba wana ari kubwa ya ushindi hivyo watapambana ili kutwaa ubingwa.

"Tunakwenda kupambana kwaajili ya kutwaa ubingwa. Gor Mahia imefanya vizuri kwenye mechi zilizopita lakini fainali itakuwa ya aina yake," alisema Tshabalala.