Tottenham ya Pochettino yaikwanyua PSG mabao 4-2

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha Kocha Mauricio Pochettino kimeanza vyema mechi yake ya kwanza kati ya tatu  za maandalizi ya msimu inazotakiwa kucheza Marekani.

Klabu ya Tottenham imeifunga PSG, kwa mabao 4-2 kwenye mechi yake ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya iliyopigwa Orlando nchini Marekani.

Kikosi hicho cha Kocha Mauricio Pochettino kimeanza vyema mechi yake ya kwanza kati ya tatu  za maandalizi ya msimu inazotakiwa kucheza Marekani.

Mabingwa hao wa Ufaransa, PSG  walikutana na kichapo hicho ikiwa ni kipindi ambacho inatajwa kufanya usajili wa mchezaji wa Barcelona, Neymar.