Tottenham, Liverpool hapatoshi leo

Muktasari:

Tottenham iliitambia Liverpool msimu uliopita kwa kuchukua pointi nne baada ya kushinda mabao 4-1 nyumbani Wembley kabla ya kutoka sare ya mabao 2-2, Anfield

London, England. Sijui nani atakuwa na bahati kuliko mwenzie. Mwamuzi Michael Oliver ndiye atachezesha pambano la leo mchana kati ya Tottenham na Liverpool katika dimba la Wembley na tayari mashabiki wa pande zote mbili wamechanganyikiwa kwa uteuzi huo.

Oliver ana bahati na timu zote mbili na mashabiki hawajielewi mpaka sasa. Mashabiki wa Tottenham ambao watakuwa nyumbani walianza kushangilia lakini walipotajiwa bahati ambayo Liverpool wanaipata kwa mwamuzi huo wakaishia kuchanganyikiwa.

Tottenham wameshinda mechi nane mfululizo ambazo mwamuzi huyo alishika filimbi kuamua mechi zao. Kama vile haitoshi, mpaka sasa Chelsea imeshinda mechi 18 katika mechi 29 ambazo mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 33 amechezesha.

Liverpool imeonekana kuwa na bahati mbaya na mwamuzi huyo ambapo katika mechi 33 alizowachezesha wamefanikiwa kushinda mechi 14 tu ambazo ni chini ya nusu ya mechi ambazo amewachezesha katika michuano mbalimbali.

Hata hivyo Liverpool imeonekana kuwa na bahati na mwamuzi huyo linapokuja suala la penalti. Oliver amewapa Liverpool penalti saba katika mechi tisa za mwisho ambazo amewachezesha. Penalti ya mwisho kabisa ni ile dhidi ya Crystal Palace ambayo ilizua utata mkubwa huku kocha wa Palace, Roy Hodgon akiilalamikia.

Tottenham inaingia uwanjani bila ya mastaa wake wawili, kipa Hugo Lloris na kiungo, Delle Alli ambao ni majeruhi huku wakiwa na kumbukumbu ya kichapo cha mabao 2-1 walichopokea ugenini kwa Watford kabla ya ratiba ya mechi za kimataifa.

Liverpool wameingia katika Ligi kwa kasi kama ilivyotazamiwa huku wakishinda mechi zote nne walizocheza mpaka sasa na kuruhusu bao moja tu katika mechi hizo. Bao hilo ni lile ambalo kipa wao, Alisson Becker aliruhusu kizembe katika pambano lililopita dhidi ya Leicester City.

Tottenham waliitambia Liverpool msimu uliopita kwa kuchukua pointi nne baada ya kushinda mabao 4-1 katika pambano la kwanza lililofanyika Wembley kabla ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika pambano kali na la kusisimua lililochezwa Anfield.

Wakati Tottenham wakiingia bila ya mastaa wao wawili, Liverpool wametumia nguvu ya pesa kuhakikisha wanakuwa na kikosi kamili katika mechi hii baada ya kuwatumia ndege binafsi mastaa wao watatu wa kimataifa wa Brazil waliokuwa katika mechi za kimataifa.

Matajiri wa klabu hiyo wamewatumia ndege binafsi mastaa wao, kipa Alisson Becker, kiungo Fabinho na mshambuliaji, Roberto Firmino ambao walikuwepo nchini Marekani kwa ajili ya kucheza pambano la kimataifa la kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo.

Mastaa hao walikuwa na mechi Jumatano usiku na kutokana na tofauti ya muda wa saa baina ya Marekani na Uingereza ilikuwa haitazamiwi kama wangewahi kurudi mapema lakini hata hivyo walifanikiwa kurudi juzi Alhamisi na jana Ijumaa walitazamiwa kufanya mazoezi na wenzao kama kawaida huku wakitazamiwa kusafiri mpaka