Tegete, Humud waibukia Majimaji

Muktasari:

  • Majimaji iliyonusurika kushuka daraja imepania kufanya vizuri msimu ujao baada ya kuwaongeza wachezaji hao.

Majimaji imefanya usajilj wa wachezaji 16 akiwamo mshambuliaji Jerry Tegeta, viungo Abdulrahman Humud na Seleman Kassim Selembe.

Majimaji iliyonusurika kushuka daraja imepania kufanya vizuri msimu ujao baada ya kuwaongeza wachezaji hao.

Mbali ya nyota hao wa Simba na Yanga pia Majimaji imemsajili mshambuliaji Danny Mrwanda, Jaffar Mohammed, Andrew Ntala, Tumba Sued, Sixnon Mwasekaga,  Mpoki Mwakinyukile na Saleh Malande kila mmoja amesaini mkataba wa mwaka mmoja.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Steven Ngonyani alisema pia wamewapa mikataba mipya nyota wao Peter Mapunda, Alex Kondo, Hashim Musa, Paul Naona, Yakob Kibiga Kennedy Kipepe na  Masela Bonaventure.

Ngonyani alisema wachezaji Hassan Hamiss, Idrisa Mohamed na Hashim Musa watasaini mikataba muda wowote kuanzia sasa.

Timu hiyo inatarajia kuanza mazoezi yao Ijumaa  hii chini ya kocha msaidizi Habibu Kondo.