Tanzania yateua wachezaji Mashindo ya EAC

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo timu ya Tanzania imetangaza orodha ya majina kwa timu zitakazoshiriki Michezo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bujumbura  nchini Burundi.

 Katika orodha hiyo  wapo viongozi maofisa wa serikali wane ambapo kutakuwa na daktari, meneja, kiongozi wa msafara pamoja na mkuu wao.

Katika Riadha kutakuwa na wanamichezo nane pamoja na kiongozi wao na kocha.

Timu ya mpira wa miguu itakuwa na wachezaji 18 pamoja na bechi la ufundi la watu watano.

 Upande wa Karate ina wanamichezo sita pamoja na mwalimu wao akiwa wa saba.

Netiboli itakuwa na wachezaji 12 pamoja na viongozi wao wawili akiwamo kocha.