Tanzania yaibuka kidedea nafasi ya pili Kombe la Dunia la watoto

Muktasari:

  • Timu hiyo iliingia hatua ya nusu fainali kwa kuibamiza Marekani kwa jumla ya mabao 5-0 katika mchezo wao war obo fainali na katika mchezo wake wa nusu fanali iliifunga Uingereza kwa mabao 2-1 na kutinga fainali hiyo.

Dar es Salaam. Timu ya wasichana wa Tanzania wanaoishi katika mazingira magumu, imemaliza katika nafasi ya pili kwenye mashindano ya Kombe la Dunia kwa watoto, mchezo uliofanyika leo Jumatano saa 5 asubuhi jijini Moscow, Urusi baada ya kufungwa na Brazil bao 1-0.

Timu hiyo iliingia hatua ya nusu fainali kwa kuibamiza Marekani kwa jumla ya mabao 5-0 katika mchezo wao war obo fainali na katika mchezo wake wa nusu fanali iliifunga Uingereza kwa mabao 2-1 na kutinga fainali hiyo.

Tanzania imeweka rekodi ya kipekee kwa nyavu zake kutikiswa mara chache, ambao imefungwa mabao matatu pekee kwenye mashindano hayo.

Vinaja hao wa Tanzania waliingia kwenye mechi hiyo  ya fainali wakiwa na ari kubwa ya kunyakua ubingwa, lakini matokeo hadi mwisho wa mchezo Brazil ndio waliibuka kidedea.

Timu hiyo inatarajiwa kuwasili nchini Jumamosi saa 9 mchana na kupokewa na wadau mablimbali wa michezo hapa nchini.

Vijana hao wa Tanzania walipokea  zawadi ya kombe pamoja na medali ya fedha kwa wache