Tanzania kuivaa Kenya, Uganda kuogelea Afrika

Muktasari:

  •  Mwenyeji Tanzania imepewa nafasi ya kuwa na timu mbili wakishindana na waogeleaji kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Sudan na Kenya.

Tanzania itawakilishwa na timu mbili za kuogelea katika michezo ya kanda ya tatu ya kuogela ya Afrika yaliyopangwa kuanza Alhamis hii katika bwawa la Hopac jijini Dar es Salaam.

 Mwenyeji Tanzania imepewa nafasi ya kuwa na timu mbili wakishindana na waogeleaji kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Sudan na Kenya.

Katibu Mkuu wa Chama Cha kuogelea Tanzania (TSA) Ramadhan Namkoveka alisema timu ya kwanza imepewa jina la Tanzanite ambayo itakuwa na jumla ya wachezaji 30 na ya pili inajulikana kwa jina la Platinum ambayo itakuwa  na wachezaji 21.

 Namkoveka alisema kuwa timu ya Tanzanite itakuwa na wachezaji 15 wanaume na 15 wanawake na ile ya Platinum itakuwa na wachezaji tisa wanawake na 12 wavulana.

 Timu hizo zipo kambini hotel ya Giraffe chini ya makocha, Alexander Mwaipasi na Michel Livingstone na zinafanya mazoezi yake kwenye bwawa la Hopac kila siku.

  Wachezaji wanaoumda timu ya Tanzanite ni Rania Karume , Chichi Zengeni, Maia Tumiotto, Smriti Gokarn (Sonia Tumiotto, Anjani Taylor ambao wote wanatoka klabu ya DSC, huku wengine ni Natalie Abwooli Sanford (MIS), Anna Guild, Emma Imhoff (MSC), Sanne Kleinveld ( ISM Moshi),  Angelica Spence, Tara Behnsen, Tami Triller,Kayla Gouws na Amani Doggart ambao wanatoka klabu ya Taliss.

 Wachezaji wanaume ni Judah Miller, Elia Imhoff, Delvin Barick, Caleb O'Sullivan, Khaleed Ladha na Matthew Guild wanatoka klabu ya Mwanza, Chris Fitzpatrick (ISM Moshi), Marin DE Villard (DSC), Adil Bharmal, Hilal Hilal, Harry McIntosh, Dhashrrad Magesvaran (Taliss) na wanaotoka klabu ya shule ya kimataifa ya Morogoro ni   Joseph Sumari, Collins Saliboko na Dennis Mhini.

Wachezaji wanaounda klabu ya Platinum kwa upande wa wanawake ni  Shivan Bhatt, Natalia (Taliss), Charlotte Sanford,  Vanessa Dickson (MIS), Rebecca Guild, Meredith Boo (MSC), Maria Bachmann ( ISM Moshi), Kayla Temba na Maya Somaiya  ambao wote wanatoka klabu ya DSC.

Wanaounda timu ya wanaume ni Aravind Raghavendran, Mohameduwais Abdullatif (Bluefins), Abraham Kayugwa( ISM Moshi), Terry Tarimo,  Aliasgar Chakera(Taliss), Zeke Boos (MSC), Yuki Omari, Augustino Lucas (Champion Rise), Fallih Ahmed (Taliss), Carter Helsby (MSC), Ian Lukaza(ISM) na Emmanuel Stenson wa shule ya kimataifa ya Morogoro.

 Namkoveka alisema kuwa mchezaji  Hilal Hilal ambaye yupo kambini Dubai atajiunga na wenzake kesho katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania, Swissair, JCDecaux,  Coca Cola, Label Promotions , Print Galore na Slipway Hotel.