TFF yapiga marufuku vitu vya ncha kali mechi ya Simba

Wednesday May 16 2018

 

By HABARI MPYA

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao ameagiza mashabiki watakaoingia Uwanjani Jumamosi kuacha kubeba kitu cha inaina yeyote ambacho kinaweza kuhatarisha usalama kwenye uwanja huo.

Mtendaji huyo wa TFF, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni pamoja na kuthibitisha ujio wa Rais John Magufuli kwenye mechi ya Simba na Kagera Sugar.

Kidao alisema wapenzi na mashabiki wanatakiwa kuacha nyumbani kitu chochote ambacho kinaweza kuhatarisha usalama kwani ulinzi utaimarisha na vyombo vya usalama.

Mashabiki wa Simba wanasubiri siku hiyo kwa shauku kutokana na kuukosa ubingwa huo kwa takriabni miaka 5 sasa.