TFF yamfungia meneja Simba mwaka mmoja

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya TFF, Wakili Iddi Mbwezeleni alisema Richard amekutwa na hatia ya makosa mawili ambayo ni kuhujumu timu ya taifa na kudharau maagizo ya mamlaka za juu yake.

Dar es Salaam. Kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia meneja wa Simba, Robert Richard kutojihusisha na shughuli zozote za soka kwa kipindi cha mwaka mmoja na faini ya Sh 4 milioni kwa kumkuta na hatia ya makosa ya kimaadili.

Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya TFF, Wakili Iddi Mbwezeleni alisema Richard amekutwa na hatia ya makosa mawili ambayo ni kuhujumu timu ya taifa na kudharau maagizo ya mamlaka za juu yake.

"Makosa aliyofanya ni mawili na kila moja lina adhabu yake ambazo adhabu hizo ukiziunganisha pamoja ndipo unapata hiyo aliyopewa.

Adhabu ya kila kosa ni faini ya Sh 2 milioni na kifungo cha kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha miezi sita," alisema Mbwezeleni.