TFF yaipeleka Yanga Cecafa

Muktasari:

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanzia kutimua vumbi Juni 29 mpaka Julai 13, 2018 jijini Dar es Salaam, sababu za Yanga kujitoa katika mashindano hayo ni kufanya maandalizi kwa ajili ya michunao ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia FC ya Kenya, Julai 18, 2018 jijini Nairobi.

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania Bara limesema limepokea barua ya Yanga kuhusiana na kujitoa kushiriki katika Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki (Kagame Cup), kwa sasa wanasubiri majibu kutoka Cecafa.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanzia kutimua vumbi Juni 29 mpaka Julai 13, 2018 jijini Dar es Salaam, sababu za Yanga kujitoa katika mashindano hayo ni kufanya maandalizi kwa ajili ya michunao ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia FC ya Kenya, Julai 18, 2018 jijini Nairobi.

Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema wameipokea barua na wamewasiliana na waandaaji wa mashindano hayo hivyo wanasubili majibu nini kitaamuliwa kufuatia kujitoa kwa timu hiyo.

"Hatuna mamlaka yoyote ya kulizungumzia suala hilo ila tumefanya mawasiliano na waandaaji wa mashindano hayo Cecafa wao ndio watakuwa na majibu ni hatua gani zinafuata bado hatujapata majibu tukipata tutaweka wazi," alisema Ndimbo.

Ndimbo aliongeza timu nyingine zimethibitisha kushiriki mashindano hayo zinatakiwa kufanya maandalizi kwa lengo la kuonyesha ushindani ili kuendelea kuboresha na kuonyesha umuhimu wa mashindano hayo.