TAKWIMU: Croatia v England, huku Luca Modric, kule Harry Kane

Muktasari:

  • Majira ya saa tatu ya usiku wa leo, Uwanja wa Luzhniki utafurika. Runinga zote kote duniani, zitakuwa zinaonesha kitu kimoja, mechi ya kukata na shoka ya nusu fainali ya pili ya Kombe la Dunia 2018, kati ya Croatia na England. Hatumwi mtu dukani wallahi!

Moscow, Russia. Baada ya kupatikana kwa mbabe kati ya Ubelgiji na Ufaransa, uso wa dunia utageuka kutoka St. Petersburg, kuelekea mji mkuu wa Moscow. Safari ya masaa nane na dakika 48, takribani kilomita 714.1 itahusika kuwatoa mashabiki 81,000 kutoka St. Petersburg, kwenda kuujaza uwanja wa taifa.

Majira ya saa tatu ya usiku wa leo, Uwanja wa Luzhniki utafurika. Runinga zote kote duniani, zitakuwa zinaonesha kitu kimoja, mechi ya kukata na shoka ya nusu fainali ya pili ya Kombe la Dunia 2018, kati ya Croatia na England. Hatumwi mtu dukani wallahi!

Unaweza kujiuliza ni kwanini mechi hii, inaonekana kuwa na ushindani mkubwa kiasi hicho. Kwa kifupi ni kwamba, mchezo huu unakutanisha mafahali wawili wenye historia ya kusisimua. Kivipi? Tulia hapo ulipo na kuiruhusu Mwanaspoti ambayo imekuwa mstari wa mbele kukupasha takwimu na taarifa muhimu kutoka Russia, ifanye kazi yake.

 

Ni hivi, rekodi zinaonesha kuwa, mara ya mwisho, England ilipofuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hii mikubwa duniani, Croatia ndio kwanza ilikuwa inahangaika kutafuta uhuru wake, kutoka umoja wa Yugoslavia, achilia mbali kufikiria kuwa na timu ya taifa.

Namaanisha, katika soka, Croatia ni watoto wadogo sana kwa England. England wakiongozwa na Malkia wao, Bibi Elizabeth wa tatu, usiku wa leo wanakutana Croatia na Rais wao, Mwanamama Kolinda Grabar-Kitarović, katika dimba la  Luzhniki, wakiwa na shauku kubwa inayosumbua nyoyo zao.

Wababe hawa wanaingia Luzhniki wakiwa na shauku ya kuweka rekodi mbili tofauti. Wakati Croatia wao wataingia katika mchezo huu wakiwa na shauku ya kutinga fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya soka lao, England watakuwa na nia ya kutoa gundu la miaka 52 ya kulikosa kombe hili. Patachimbika aisee!

Turudi nyuma kidogo. Wakati Kocha wa Croatia anachukua mikoba ya ukocha katika timu ya taifa ya Croatia (2017), alikuwa na kibarua cha kupata mfumo mzuri ambao ungemruhusu kuwatumia moja ya viungo bora duniani kwa sasa bila tabu. Nawazungumzia Luca  Modric (Real Madrid) na Ivan Rakitic (Barcelona).

Akaamua kutumia mfumo wa 4-2-3-1, ambapo Modric alikabidhiwa mikoba ya kucheza namba 10, yaani kiungo mshambuliaji, nafasi ambayo ni tofauti na anayocheza akiwa Real Madrid. Japo Modric ahusiki sana kuichezesha kwa mfumo huu, mashambulizi, amekuwa msaada kwa washambuliaji na wakati mwingine akicheza kama 'false number 9'.

Mfano mzuri ni mechi yao dhidi ya Argentina. Alitupia wavuni katika ushindi wa 3-0. Modric aligusa mpira mara 62, akipiga pasi 42 tu kwenye mchezo huu, lakini katika mchezo wa robo fainali, mguu wa nahodha huyo, uligusa mpira mara 139, akipiga pasi 102.

Mbinu hii ikitumika leo, England hawatokuwa salama! Nasema wajukuu wa Malkia watapata tabu sana pale Luzhniki. Ukiachana na viungo hawa, kikosi cha Croatia kinajivunia uwepo wa Madam Rais Kolinda huko jukwaani (habari zake tulishaziandika mbona), bila kusahau wachezaji wazoefu wanaokipiga kati…