Ruby: Sipendi kufananishwa na Nandy

Muktasari:

  • Ruby na Nandy ni wanamuziki wanaoimba kwa mitindo na sauti zinazofanana kidogo.

Dar es Salaam. Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ruby amewataka watangazaji na waandishi wa habari kuacha kuuliza kuhusu Nandy kama maswali yameisha.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ruby anasema hapendezwi na maswali hayo na kusema kuwa ni kama wanataka kuchochea ugomvi wakati yeye hayupo huko kwa sasa anaendelea kupambana na hali yake.

“Nachukia sana swali la kufananishwa na Nandy kwa sababu nimechoka aisee, Ni kama vile watangazaji wanashindwa ni maswali gani kuuliza sababu mahojiano ni yangu vipi uanze kuniuliza maswali kuhusu Nandy.”

“Nampenda Nandy, ni msanii mzuri na anaimba vizuri sana lakini sipendi kuniuliza maswali mengi kumuhusu yeye kwani maswali kwangu yameisha,” aliongeza

Ruby kwa sasa anasema yupo anaandaa nyimbo zake siyo muda mrefu ataanza kuziachia na kusema mashabiki zake wakae mkao wa kula.

“Kuna nyimbo nyingi zinakuja watu waendelee kusubiri tu, mambo mazuri yanakuja,” alisema Ruby.