Azam kumpeleka Sure Boy Singida United

Muktasari:

Chanzo hicho kilisema bado Azam wana kigugumizi juu ya kumuachia fundi huyo wa mpira kwani bado hawajapata mbadala wake, huku kiungo mwenzake, Himid Mao akiwa mbioni kujiunga na Bidvest Wits ya Afrika Kusini.

Kuna habari za chinichini, kwamba Azam FC, walitaka kumpeleka kiungo wao Salum Abubakar 'Sure Boy' kwa mkopo Lipuli ya Iringa, lakini amewagomea na kuwaambia wampeleke Singida United.
Chanzo hicho kilisema bado Azam wana kigugumizi juu ya kumuachia fundi huyo wa mpira kwani bado hawajapata mbadala wake, huku kiungo mwenzake, Himid Mao akiwa mbioni kujiunga na Bidvest Wits ya Afrika Kusini.
"Kuna mchezaji wanahitaji achukue nafasi ya Sure Boy, lakini bado hawajamalizana naye ndio maana unaona hizo habari bado zipo chini kwa chini," kilisema chanzo hicho.