Sugu kuishtaki Basata kwa kuufungia wimbo wake

Muktasari:

Amesema katika kesi hiyo ataongozwa na mawakili sita

Dodoma. Mwanamuziki Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ambaye ametoka jela hivi karibuni amelieleza Bunge leo Jumatano Juni 20, 2018 kwamba atatumia mawakili sita kulifungulia mashtaka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kupinga kufungiwa wimbo wake wa #219.

Akizungumza katika mjadala wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 bungeni leo Juni 20,  2018, Mbilinyi amesema kila taasisi imegeuka kuwa polisi ikiwemo Basata walioufungia wimbo huo uliovuja, kabla ya kuutoa rasmi.