Straika wa Uingereza arudi kisa Samatta

Muktasari:

  • Mchezaji huyo alisema kwamba aliongea na Samatta kuhusu kushiriki katika tukio hilo, ambapo aalipohakikishiwa aliamua kujiunga na nyota wenzake.

Dar es Salaam. Mshambuliaji Adi Yusuf anayekipiga katika kikosi cha Solihull Moors Fc kinachoshiriki Ligi Daraja Kwanza England amejikuta kuguswa na kitendo cha mshambuliaji Mbwana Samatta cha kuchangisha  pesa kwaajili ya Shule za Msingi.

Mchezaji huyo alisema kwamba aliongea na Samatta kuhusu kushiriki katika tukio hilo, ambapo aalipohakikishiwa aliamua kujiunga na nyota wenzake.

"Niliongea na Samatta akanambia kwamba  kuna kitu cha muhimu anakifanya kwahiyo nikaona nije, hapa unaponiona nina masaa matatu  tangu nishuke katika Ndege ndio maana nimechelewa uwanjani hata kucheza pia," alisema.

Yusuph ambaye naye amekuwa akiendesha hisani yake ya kusaidia watoto na watu wasiojiweza, alisema anaendelea nayo na ana lengo la kuitanua zaidi.