Straika Stand ajiweka sokoni kimtindo

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba alijiunga na Stand United kwenye dirisha dogo la usajili akiwa kama mchezaji huru.

Mwanza. Baada ya kumaliza mkataba wake na Stand United,mshambulijai Abdallah Juma amesema kwa sasa yuko huru kujiunga na klabu yoyote ya Ligi Kuu.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba alijiunga na Stand United kwenye dirisha dogo la usajili akiwa kama mchezaji huru.

Juma alisema kwa sasa yuko huru baada ya kumaliza mkataba wake na Stand United hivyo anakaribisha mazungumzo na timu nyingine za Ligi Kuu.

“Mkataba wangu umeshamalizika Stand United nilisaini wa miezi sita ili kumalizia ligi na sasa niko huru kuzungumza na klabu yoyote,”alisema Juma.

Alisema pia bado anakaribisha mazungumzo na mabosi wa Stand United kwani katika kipindi alichokaa na timu hiyo amefanya kazi nao vizuri.

“Nimefanya nao kazi vizuri hivyo sitasita kama wakinipa mkataba mmoja kwa kuwa Stand United ni timu nzuri”alisema Straika huyo ambaye pia alishawahi kukipiga kwenye klabu ya Mtibwa Sugar.