Straika Simba bado hakijaeleweka Singida

Muktasari:

Pastory aliliambia Mwanaspoti kuwa awali alishafanya mazungumzo na uongozi wa Singida, lakini kutokana na kuwa na mkataba aliwaambia viongozi hao wamalizane na Simba.

STRAIKA wa Simba, Pastory Athanas yupo mbioni kujiunga na klabu ya Singida United iliyopanda Daraja na itashiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza msimu ujao.

Pastory aliliambia Mwanaspoti kuwa awali alishafanya mazungumzo na uongozi wa Singida, lakini kutokana na kuwa na mkataba aliwaambia viongozi hao wamalizane na Simba.

“Bado nina mkataba na Simba, niliwaachia viongozi wa Singida kazi ya kuzungumza nao lakini leo (jana Jumatano) wameniita ila bado sijajua kama natoka kwa mkopo au wananichukua jumla jumla,” alisema

Pastory aliongeza kuwa haangalii sehemu ya kufanyia kazi na kama dili hilo likienda sawa atajitahidi kutumia nafasi hiyo kusahihisha makosa aliyofanya msimu uliopita kwa kuonyesha kiwango duni.