Stars yarejea leo akili yote kwa DR Congo

Muktasari:

Timu hizo mbili zinajiandaa na mashindano ya kusaka kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2019

Dar es Salaam. Taifa Stars inategemewa kuwasili nchini leo saa 9 Alasiri wakitokea Algeria walipocheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na kufungwa mabao 4-1.

Taifa Stars itaingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya DR Congo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Jumanne ijayo.

Taifa Stars na DR Congo wamekutana mara tano tangu 1995, mara mbili katika mechi za mashindano na mara tatu katika michezo ya kirafiki.

Tanzania imeshinda mechi mara mbili, sare moja na kufungwa mechi mbili mara ya mwisho zilipokutana Februari 23, 2012 timu hizo zilitoka suluhu.

Kikosi hicho kitaundwa na makipa, Aishi Manula (Simba), Ramadhani Kabwili (Yanga), Abdulraham Mohammed (JKU).

Mabeki ni Shomari Kapombe (Simba),Hassan Kessy (Yanga),Gadiel Michael (Yanga),Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda (Baroka), Erasto Nyoni (Simba).

Viungo ni Hamisi Abdallah (Sony Sugar), Mudathir Yahya (Singida United), Said Ndemla (Simba), Faisal Salum (JKU), Abdulazizi Makame (Taifa Jang'ombe), Farid Mussa (CD Tenerife), Ibrahim Ajib (Yanga), Shiza Kichuya (Simba) Mohammed Issa (Mtibwa Sugar) na Thomas Ulimwengu.

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk), Saimon Msuva (Difaa El Jadida), John Bocco (Simba),Zayd Yahya (Azam).