Stand United, Alliance ngoma ngumu

Muktasari:

Mechi hizo ni kuendelea kujipima nguvu kwa klabu hizo kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu itakayoanza kutimua vumbi Agosti 22.

Mwanza. Stand United imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Alliance FC katika mchezo wa kirafiki uliopigwa leo Jumanne kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini hapa.

Stand United  ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 34 kupitia kwa mshambuliaji Bigirimana Blaise kabla ya wenyeji Alliance kusawazisha dakika za nyongeza kupitia kwa Martin Kigy.

Kwa matokeo hayo, Alliance ilifanikiwa kutwaa kombe kupitia kwa waandaaji wa mashindano hayo ya 'Pre-season' kampuni ya Cleveland chini ya mkurugenzi Kabole Kahungwa.

Mechi hizo ni kuendelea kujipima nguvu kwa klabu hizo kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu itakayoanza kutimua vumbi Agosti 22.