Snura, Sultan King kuipamba Taifa Moja Iddi
Muktasari:
Pili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar
Dar es Salaam. Mwanamuziki Snura na Sultan King watatumbuiza katika tamasha la kampeini ya Taifa Moja litakalofanyika Zanzibar siku ya Iddi Pili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Tamasha hilo linalengo ya kutoa elimu kwa Wananchi kupitia burudani juu ya uhuru wa kutuma pesa bila mipaka na ushirikiano wa makampuni matatu ya simu za mkononi kupitiia huduma zao TigoPesa, Airtel Money na Ezy Pesa.
Mratibu wa tamasha hilo Mkurugenzi wa kampuni ya Fern Tanzania, Liginiku Millinga alisema maandalizi yote yamekamilika na kuwaomba wakazi wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi kupata burundani kutoka kwa wasanii hao pamoja na kupata elimu juu ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao wowote hapa Tanzania kwa gharama ile ile.
Millinga alisema sasa ni zamu ya Zanzibar siku ya Iddi Pili kwenyeviwanja vya Mnazi Mmoja watashudia burudani kutoka kwa Snura pamoja na Sultan King.
"Tangu tuanze kampeni yetu ya Taifa Moja tumepata mafanikio mengi na kufikisha ujumbe wetu wa uhuru wa kutuma pesa bila mipaka kupitia burudani kutoka kwa wanamuziki mbalimbali," alisema Millinga.
Hayo makampuni ya simu za mkononi wameamua kuungana na taifa moja katika kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha.
Millinga aliongeza hali hii imewafanya Watanzania kutokuwa na wasiwasi tena pale anapotaka kutuma pesa kwani hanakuwa na uhuru wa kutuma pesa kwenda mtandaowowote kwa gharama ile ile.