Singida United yanasa wachezaji sita wapya

Muktasari:

Timu hiyo inashiriki mashindano ya mapinduzi kwa mara ya kwanza msimu huu

Dodoma. Wakati dirisha la usajili likifungwa saa 6 usiku wa Ijumaa, Uongozi wa Singida United umethibitisha kuwasajili wachezaji wasita wakiwemo nyota wa kikosi cha Serengeti Boys.

Wachezaji wa Serengeti Boy waliojifunga Singida United ni  aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Issa Abdi Makamba, Ally Ng'anzi, Asad Juma na Mohamed Abdallah wamesajiliwa kwa lengo la kuendeleza vipaji vyao.

Mbali na makinda hao pia Singida United imemsajili mshambuliaji wa Danny Lyanga kwa mkataba wa miaka mwili akiwa mchezaji huru akitokea Oman.

Katika kuhakikisha inaziba vyema pengo la washambuliaji  Atupele Green na Pastory Athanas, timu hiyo imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji Mkongo Kambale Salita au Papy Kambale kutoka Etincelles ya Rwandwa.