Atupele Green , Pastory Athanas waachwa Singida United

Muktasari:

  • Atupele alisajiliwa na Singida ya kocha, Mholanzi Hans Pluijm akitokea  JKT Ruvu, wakati Athanas alikuwa Simba.

KLABU ya Singida United,  imethibitisha kuachana na mastraika wake, Atupele Green na Pastory Athanas,  wakati Frank Zakaria na Mohamed Titi wanapelekwa kwa mkopo Stand United.

Mratibu wa timu hiyo, Festo Sanga amesema, wamewaacha wachezaji hao kwa madai ya changamoto ya ushindani wa namba, hivyo nafasi zao wanafikiria namna ya kuziziba.

"Atupele Green na Athanas wapo huru lakini Zakaria na Titi, tumewapeleka Stand United wakaangalie changamoto nyingine, ubora wa viwango vyao ndivyo vitakavyowarudisha kwenye timu,"alisema Sanga.

Atupele alisajiliwa na Singida ya kocha Mholanzi Hans Pluijm akitokea JKT Ruvu wakati Athanas alitokea Simba.

Kwa upande wa Atupele ambaye alisajiliwa na Singida mwanzoni mwa msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili na sasa anafanya mazoezi Uwanja wa Sinza Star alisema:" Mimi sasa hivi ni mchezaji huru, nimemalizana na Singida kwa makubaliano maalumu tukavunja mkataba.