Msuva aibeba Taifa Stars kila kona

Muktasari:

  • Afunga mechi mbili alizoitwa, huku akiwaomba wachezaji wa Bongo kuchangamkia fursa za kucheza nje ili kuwa na wachezaji idadi kubwa wanaocheza nje ya nchi.

Dar es Salaam. Winga wa zamani wa Yanga, Saimon Msuva anayecheza soka la kulipwa nchini Morocco katika klabu ya Difaa El Jadid, amesema kuwa kucheza soka nje ya Tanzania ndio kumefanya kuwa mcheza mwenye uwezo kuliko wakati anacheza hapa.

Morocco kuna ushindani wa kweli na hata ligi yao pamoja na mashindano mingine yana timu ambazo ukikutana nazo lazima upate ushindani na hapo ndio chanzo cha mimi kuzidi kuimarika kisoka.

“Nashukuru kuwa na rekodi nzuri ya kufunga mabao matatu katika mechi mbili nilizocheza nikiwa na Taifa Stars kwa mara ya kwanza nikiitwa nikiwa natokea nje ya Tanzania,” alisema.

“Naomba Mungu anisaidie ili kuweza kuongeza rekodi yangu hii kwa Stars nikiitwa kutokea nje, lakini nawaomba wachezaji wanzangu ambao wenye uwezo wakipata nafasi ya kwenda nje wasipuuze kwani tukiwa wengi tunaocheza nje tutakuwa na timu ya Taifa bora,” alisema Msuva.