Simba yawashukuru wadhamini SportPesa

Wednesday May 16 2018

 

Dar es Salaam. Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema anawashukuru wadhamini wao SportPesa kwa udhamini mnono waliowapa, jambo lililofanikisha kulipa mishahara ya wafanyakazi kwa wakati.

Manara alisema kwa namna ya kipekee SportPesa wamekuwa chachu ya mafanikio yao ya kutwaa Ubingwa msimu wa 2017/18 kutokana na udhamini wa Sh1 bilioni moja ambao wanawapatia kwa mwaka.

Manara alimpongeza Tarimba Abbas ambaye ni Mkurugenzi wa SportPesa kutokana na udhamini huo kwa klabu ya Simba ambao pia umewaqwezesha kusajili wachezaji wa gharama kubwa waliowahitaji.

Simba imetwaa ubingwa msimu huu na inatarajiwa kukabidhiwa kombe la ubingwa na Rais John Magufuli kwenye mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumamosi.