Simba yawapongeza wachezaji, benchi la ufundi kutwaa ubingwa

Wednesday May 16 2018

 

Dar es Salaam. Uongozi wa Simba umewapongeza wachezaji wa klabu hiyo kwa kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Hayo aliyasema Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kwenye mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Serena Hoteli.

Manara alisema wamejipanga vyema kuhakikisha kwamba Simba inamaliza msimu huu bila kufungwa mechi yoyote, huku wakitambua kwamba Kagera Sugar ina kikosi kizuri, hivyo wamejipanga kuwakabili.

Msemaji huyo aliongeza kuwa, anawapongeza benchi la ufundi kwa umakini wao wa hali ya juu kuhakikisha timu hiyo haijapoteza mechi ikiwa ni mkakati wao msimu huu.