Simba yauteka uwanja wa Nangwanda

Muktasari:

Mechi ya Simba na Ndanda FC itachezwa majira ya saa 10:00 jioni ikiwa ni mwendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Bara.

Mtwara. Sehemu kubwa ya mashabiki wa soka waliofika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara asubuhi na mapema kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa Simba na Ndanda FC ni wa Wekundu wa Msimbazi tofauti na ilivyo kwa wenyeji.

Mashabiki hao waliokuwa wamevalia mavazi yenye rangi nyekundu na nyeupe, walianza kufurika uwanjani hapo kuanzia majira ya saa 2:00 asubuhi hiyo kabla hata tiketi hazijaanza kuuzwa.

Walizidi kumiminika zaidi uwanjani baada ya kuyaona magari ya kuuza tiketi na haraka wakapanga mistari bila kushurutishwa ili wapate huduma hiyo.

Kabla, walikuwa wakifanya kazi ya utalii kwa kuzunguka uwanja huku na kule.