Simba yatua kuweka heshima Songea

Dar es Salaam. Wachezaji wa Simba wamewasili mijini Songea kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji FC utakaopigwa leo Jumatatu.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara, Simba wamewasili Songea juzi Jumamosi huku wakiwa na wachezaji wengi wa kikosi cha pili.
Timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi wameamua kupeleka wachezaji wengi wa kikosi cha pili, huku wengine wamebaki Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya SportPesa Super Cup.
Michuano hiyo inatarajia kuanza Juni Nairobi, Kenya  na itakayoshirikisha timu zote ambazo zinazodhaminiwa na Kampuni hiyo.
Kuelekea mchezo na Majimaji, Simba wametamba kupambana ili waweze kupata pointi tatu.