Simba yasaka stamina ufukweni

Muktasari:

Mabingwa hao wa Kombe la FA wamedhamilia mwaka huu kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu na kufanya vizuri mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika

Dar es Salaam. Simba imeendelea na mikakati yake ya kujiimarisha kwa ajili ya Ligi Kuu na Kombe la Mapinduzi baada ya leo kufanya mazoezi ufukweni.

Mazoezi hayo yaliyoanza saa 2.00 asubuhi hadi 4.00 asubuhi yalisimamiwa na kocha msaidizi Masoud Djuma na Meneja Robert Richard.

Hata hivyo kundi kubwa la wachezaji wa kikosi chake halikuhudhuria kutokana na wengi kuwa kwenye majukumu ya timu za taifa na wengine mapumziko.

Djuma alisema kwa sasa msisitizo wao ni mazoezi ya kuwaweka fiti wachezaji na baada ya hapo wataingia kwenye ufundi.

"Tunataka hadi ligi itakapoendelea, wachezaji wawe katika hali nzuri kwa sababu hatutopata tena nafasi ya mapumziko marefu," alisema Djuma