Simba yawasha moto kujua kanuni za hisa

Muktasari:

Waziri Mwakyembe alibainisha kupokea barua ya Simba kuomba majadiliano na kusisitiza kwamba ndani ya siku nne kuanzia leo Jumatano wanatarajia kukutana na viongozi wa Simba.

Dar es Salaam. Wakati Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akisisitiza mfumo wa uendeshaji wa hisa kwenye unampa mwekezaji asilimia 49, uongozi wa Simba umeiandikia barua Serikali kuomba majadiliano ya kanuni za mfumo huo.
Waziri Mwakyembe alibainisha kupokea barua ya Simba kuomba majadiliano na kusisitiza kwamba ndani ya siku nne kuanzia leo Jumatano wanatarajia kukutana na viongozi wa Simba.
"Tutakutana nao kujadiliana lakini tayari tumepitisha kanuni tangu Oktoba 27 hata hivyo mazubgunzo na Simba hayawezi kuvunja kanuni," alisema Dk Mwakyembe.