Simba yanusa ubingwa Ngao ya Jamii

Muktasari:

Simba inataka kutwaa taji hilo kwa mara ya nne, wakati Mtibwa wanataka kunyakuwa kwa mara ya kwanza

Mwanza. Mabao ya Meddie Kagere na Hassan Dilunga yanaifanya Simba kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere alitumia vizuri nguvu zake kumwacha beki Hassan Isihaka wa Mtibwa  na kuifunga bao la kuongoza kwa Simba.

Dakika 32, Kelvin Sabato anaisawazishia Mtibwa Sugar kwa shuti lilogonga mwamba na kujaa wavuni.

Katika dakika za nyongeza Dilunga alifunga bao la pili kwa Simba kwa shuti lake lililomgonga beki na kujaa wavuni na kuwafanya mabingwa mara tatu wa Ngao ya Jamii kwenda mapumziko wakiwa mbele.

Awali Mtibwa Sugar imekuwa ya kwanza kuwasili uwanjani saa 8:43 huku mashabiki wa Yanga wakiwashangilia na kwenda moja kwa moja katika vyumba vya kubadirishia jezi.

Licha ya Mtibwa Sugar kuwahi uwanjani, lakini Simba ilitua kibabe baada ya kuongozwa na gari la polisi na magari mengine matatu, huku wakishangiliwa na mashabiki wao.

Simba imetua saa 8:50 wakipitia mlango mkubwa ambao ulipitwa na wapinzani wao,ikiwa na ulinzi mkali wakiwamo Askali Polisi ambao wamesimamia hadi wachezaji wanashuka kwenye gari.

Mashabiki walipoona gari la chama lao, walilipuka shangwe kubwa la kuzizima uwanja mzima.

Vikosi

Simba: Kipa Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, James Kotei, Hassan Dilunga, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya.

Akiba kipa Ally Salim, Mohammed Hussen, Shomary Kapombe, Mzamiru Yassin, John Bocco, Adam Salamba na Mohammed Rashid.

Mtibwa Sugar: Benedict Tinoco, Rodgers Gabriel, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Hassan Isihaka, Cassian Mponera, Shaban Nditi, Ismail Mhesa, Saleh Khamis, Kelvin Sabato, Awadhi Juma, Salum Kihimbwa 

Akiba: Shaban Kado, Dickson Job, Henry Joseph, Ally Makalani, Haruna Chanongo, Ayoub Semtawa, Juma Luizio