Simba yatuma ujumbe mzito kwa Yanga mechi ya watani

Muktasari:

Mabao ya Simba yamefungwa na Emmanuel Okwi, Mzamiru Yassin (2) na Laudit Mavugo jambo lililowafanya vijana hao wa kocha Omog kuendelea kubaki kileleni baada ya kujizolea pointi tatu muhimu.

Dar es Salaam. Kikosi cha Simba kimeishangaza Njombe Mji baada ya kuilima mabao 4-0 kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Jumamosi.
Mabao ya Simba yamefungwa na Emmanuel Okwi, Mzamiru Yassin (2) na Laudit Mavugo jambo lililowafanya vijana hao wa kocha Joseph Omog kuendelea kubaki kileleni baada ya kujizolea pointi tatu muhimu.
Bao la Okwi kwenye  mchezo huo limemuwezesha kufikisha mabao nane mpaka sasa kwenye Ligi Kuu.