Simba yaifuata Yanga Zanzibar

Saturday August 12 2017

 

By Fredrick Nwaka, Mwananchi

Dar es Salaam. Timu ya Simba itaondoka Jumatatu kwenda kisiwani Unguja ambako itaweka kambi ya siku nane kujiandaa na pambano la watani wa jadi dhidi ya Yanga.

Hatua hiyo ya Simba ni kama kuifuata Yanga ambayo pia imeamua kuweka kambi kisiwani Pemba kujiandaa na mchezo huo.

Mechi hiyo itaashiria mwanzo wa msimu wa Ligi Kuu 2017/18.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara alisema ikiwa huko Simba itacheza mechi moja ya kirafiki.

"Tunakwenda  Zanzibar Jumatatu baada ya kucheza na Mtibwa kesho Jumapili. Nii mechi muhimu kwetu.,"alisema Haji