Simba wajilipua kwa Okwi, Manula

Muktasari:

Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Bara mchezaji akipata kadi tatu za njano anakosa mechi moja

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi na kipa Aishi Manula uenda wataikosa mechi ya Yanga kama watapata kadi ya njano katika mchezo wa leo jioni dhidi ya Lipuli kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.

Nyota wawili wa Okwi na Manula ilitegemewa kutokuanza katika mechi hii kwa kuwa wanakadi mbili za njano na iwapo watapata kadi tu itakuwa ya tatu hivyo watakosa mechi ya watani wa jadi ya Aprili 29.

Kocha wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre amewaanzisha nyota hao bila ya kujali kama wanaweza kupata kadi za njano na kuifanya timu yake kupoteza wachezaji muhimu katika mchezo ujao dhidi ya Yanga.

Katika mchezo wa leo Mfaransa huyo ameendelea kutumia mfumo wake 3-5-2 katika kuhakikisha wanashinda na kuzidi kujikita kileleni mwa ligi hiyo.

Kikosi kitakachoanza ni kipa Aishi Manula, Nicolas Gyan, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Yusuf Mlipili, James Kotei, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Emmanuel Okwi, John Bocco na Shizza Kichuya.