Simba wafuta cheo cha Katibu Mkuu

KLABU ya Simba inaelekea kufuta cheo cha Katibu Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo.
Mwanasheria mkuu wa Simba, Wakili Msomi Evodius Mtawala alisema matakwa ya katiba mpya ya klabu hiyo ambayo itaendeshwa kwa mfumo wa kampuni, yanakiondoa Rasmi cheo hicho.
"Badala ya kuwa na katibu mkuu, majukumu ya nafasi hiyo yatatekelezwa na Mkurugenzi wa Wanachama na mashabiki," alisema Mtawala.
Mtawala alisema pia Rais wa klabu hiyo cheo chake naye kitabadilika baada ya mabadiliko hayo ambapo atakuwa ni mwenyekiti wa bodi ya kampuni.