Simba kuyatolea ufafanuzi mambo mbalimbali kesho

Muktasari:

  • Taarifa iliyotolewa na mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara leo, imeeleza kuwa mkutano huo utaanza majira ya saa sita kamili mchana ambao utafanyika katika ukumbi mdogo wa klabu hiyo jijini.

Dar es Salaam. Klabu ya Simba, kesho watakutana na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo, Msimbazi jijini kutolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu klabu hiyo.

Taarifa iliyotolewa na mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara leo, imeeleza kuwa mkutano huo utaanza majira ya saa sita kamili mchana ambao utafanyika katika ukumbi mdogo wa klabu hiyo jijini.

"Pamoja na mengine yatakayozungumzwa hiyo kesho, mkutano huu ni muhimu sana kwako/kwenu kuhudhuria kwani kuna mengi ya umuhimu ya kuyatolea ufafanuzi na kuyaweka wazi kwa umma, mashabiki na wanachama wetu kupitia kwako/kwenu," inasema sehemu ya taarifa ya Manara.

Taarifa hiyo pia imetangaza utaratibu wa kufanyika mkutano kila siku ya Jumatatu, ambao hapo awali haukuwepo.