Simba ina deni la Yanga mwezi Septemba

Muktasari:

  • Zipo ambazo zimeonyesha kugangamala ili hata ligi ikichanganya baadaye, ziwe zimesimama pazuri japokuwa kazi kLigi Kuu Tanzania Bara imeanza kwa kishindo Agosti 22 mwaka huu. Kinachofurahisha ni kwamba, timu ngeni zimeanza kwa mbwembwe lakini nyingine zimeanza kulegea mapema.ubwa bado iko mbele.

Dar es Salaam. Ligi Kuu Tanzania Bara imeanza kwa kishindo Agosti 22 mwaka huu. Kinachofurahisha ni kwamba, timu ngeni zimeanza kwa mbwembwe lakini nyingine zimeanza kulegea mapema.

Zipo ambazo zimeonyesha kugangamala ili hata ligi ikichanganya baadaye, ziwe zimesimama pazuri japokuwa kazi kLigi Kuu Tanzania Bara imeanza kwa kishindo Agosti 22 mwaka huu. Kinachofurahisha ni kwamba, timu ngeni zimeanza kwa mbwembwe lakini nyingine zimeanza kulegea mapema.ubwa bado iko mbele.

Timu zilizopanda daraja ni Coastal Union ya Tanga ambayo iko nafasi ya sita ikiwa na pointi tano sawa na JKT Tanzania ambayo pia ina pointi tano.

KMC iko nafasi ya 11 na pointi zake tatu, nafasi ya 14 iko Biashara yenye pointi tatu pia.

African Lyon ya Dar es Salaam na Alliance ya Mwanza zinaonyesha gwaride kuanza kuwaelemea mapema.

Ukiacha wageni, timu za Mbeya City na Mwadui FC ndizo zilizotia fora hadi sasa kwani hazina hata pointi. Mbeya City imecheza mechi tatu ugenini na zote imepoteza, imepigwa na Simba na Azam FC 2-0 kabla ya kulala kwa Mtibwa mabao 2-1.

Pia, Ruvu Shooting imeanza kupapaswapapaswa kwani mpaka sasa ina pointi moja, imepoteza mechi moja kwa Ndanda FC lakini ikatoka sare na KMC.

Eneo la kawaida ukiondoka kwenye tano bora, ziko timu kibao hapa kuna Yanga, Kagera Sugar ambayo imeonyesha kuwa msimu huu haitaki mchezo baada ya msimu uliopita kuharibu mbaya. Pia ziko Mtibwa Sugar, Prisons, Ndanda na Lipuli.

Kwa sasa mechi zimesimama kupisha mechi za kimataifa wikiendi hii, lakini shughuli itaendelea baada ya hapo, Yanga inarudi rasmi kwenye ligi yake na itaanza na Mwadui na African Lyon watawatoa kwa mara ya kwanza Coastal Union ya Tanga kutoka nje ya Uwanja wa Mkwakwani. Prisons itapambana na Ruvu Shooting.

Septemba 15, Lipuli itaialika Mtibwa Sugar wakati Ndanda itakuwa na kazi na Simba pale Nangwanda Sijaona huku Mbao FC ikicheza na JKT Tanzania kabla ya KMC kucheza na Singida United.

Hiyo ni sehemu moja, lakini mambo yote ni Septemba 30. Hapa hata kama ligi itakuwa inaendelea, mioyo ya wachezaji wa timu zote itasimama kwa muda kusikilizia huko taifa mambo yamekuwaje.

Siku hiyo, ndiyo siku ambayo miamba ya soka Tanzania, Yanga na Simba inacheza.

Safari hii mpambano huo unahanikizwa na usajili wa pande zote mbili, kila upande unajivunia wachezaji wake, kwa Simba kuna majina kadhaa lakini Meddie Kagere na Emmanuel Okwi yanatajwa kwa Yanga kuna Harietier Makambo na Ibrahim Ajib. Ni jambo la kusubiri.

Tangu mwaka 1980, mwaka ambao Tanzania ilicheza Fainali za Afrika kwa mara ya mwisho, Simba na Yanga zimecheza mara 10 kwa mwezi Septemba.

Hata hivyo, Yanga ndiyo wababe zaidi kwenye mwezi huo kwani wamewafunga Simba mara nne, Simba ikishinda mara tatu na kutoka sare tatu kwenye mechi za Ligi Kuu. Nje ya Ligi Kuu, Simba na Yanga hazikuwahi kukutana kwenye mwezi huo.

Mechi zenyewe hizi hapa

Simba na Yanga zilikutana Septemba 5, 1981 na katika mchezo huo, Yanga ilishinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa. Bao la Yanga liliwekwa kimiania na ‘Jenerali’ Juma Mkambi katika dakika ya 42. Mkambi kwa sasa ametangulia mbele za haki.

Mtanange mwingine ulikuwa Septemba 18, 1982. Hapa Yanga iliifanyizia Simba kwa kuirarua mabao 3-0 yakiwekwa wavuni na Omar Hussein dakika ya pili na dakika ua 85. Omari Hussein baadaye alikuja kuichezea Simba. Bao lingine lilifungwa na Makumbi Juma dakika ya 62.

Septemba 10, 1983, Yanga iliilaza Simba mabao 2-0 kupitia kwa Lilla Shomari aliyejifunga dakika ya 72 kabla ya beki wa kushoto, Ahmed Amasha kuongeza lingine dakika ya 89.

Simba na Yanga zilitoka sare 1-1 na hii ilikuwa Septemba 25, 1983. Ni kama siku maalumu kwani hata wafungaji ubini wa baba zao ni Juma. Bao la Simba lilifungwa na Sunday Juma dakika ya 72 na dakika tatu baadaye Makumbi Juma akasawazisha.

Mpambano mwingine wa timu hizo ulikuwa Septemba 26, 1993. Hapa ndipo Simba ilianza kuifunga Yanga kwa mwezi huo. Iliichapa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Dua Said katika dakika ya 13.

Miaka mitatu baadaye, yaani Septemba 21, 1996 hakukuwa na mbabe kwani mechi ya timu hizo ilimalizika kwa suluhu kabla ya Simba kuichapa Yanga 1-0, hii sasa ni Septemba 1, 2001. Mfungaji wa bao hilo pekee alikuwa Joseph Kaniki dakika ya 76.

Septemba 28, 2003 mahasimu hao walitoka sare ya 2-2. Wafungaji katika mchezo huo walikuwa Emmanuel Gabriel dakika ya 27 na 36 wakati mabao ya Yanga yaliwekwa wavuni na Kudra Omary dakika ya 42 na Heri Morris dakika ya 55.

Mpambano mwingine kwa mwezi huo ulikuwa Septemba 18, 2004 ambao Simba iliichapa Yanga bao 1-0 lililofungwa na Athumani Machuppa dakika ya 82 baada ya kumpiga chenga Samson Mwamanda na kufunga kirahisi.Septemba 26, 2015; Yanga iliitandika Simba mabao 2-0 mechi ya Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Taifa. Mabao ya washindi yalifungwa na Amiss Tambwe dakika 44 na Malimi Busungu aliyekwamisha mpira wavuni dakika 79.