Simba, Yanga zachonganishwa Kenya

Sunday June 3 2018

 

By Gift Macha

Kenya: Walichokifanya waandaaji wa michuano ya SportPesa Super Cup kwa Simba na Yanga, siyo kitu kizuri kabisa.

Waandaaji wa michuano hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa Afrika Mashariki na Kati kwa upande wa klabu baada ya ile ya Kagame, wamezichongea Simba na Yanga na kama zikiteleza tu inakula kwao.

Iko hivi. Hapa Nakuru kila timu mbili zinatumia hoteli moja ili kudumisha umoja na urafiki lakini Simba na Yanga zimewekewa mtego.

Unaambiwa wale wapinzani wa Yanga leo Jumapili, Kakamega Homeboys wamewekwa hoteli moja na Simba. Halafu mambo yako hivyo hivyo kwa Kariobangi Shawks ambao wanacheza na Simba keshoJumatatu  wamewekwa hoteli moja na Yanga.

Sasa unaambiwa Yanga ikiwa inacheza, huko kwenye hoteli ya Simba kuna shamra shamra za kutosha, na vivyo hivyo wakicheza Simba huko kwenye hoteli ya Yanga ni amsha amsha za kutosha kutoka kwa wapinzani zao hao.