Simba na Yanga raundi ya pili CAF balaa tupu!

Muktasari:

Simba wakiwafunga Wadjibout watakutana na mshindi kati ya EL Masry ya Misri watakaokutana na Green Buffaloes ya Zambia.

Dar es Salaam. Yanga itakutana na mshindi wa EL Merreikh ya Sudan watakaokutana na watakaokutana na Township ya Botswana.
Simba wakiwafunga Wadjibout watakutana na mshindi kati ya EL Masry ya Misri watakaokutana na Green Buffaloes ya Zambia.
Mapema leo mchana Jumatano, CAF imetoa droo ya mashindano ya klabu ambapo mabingwa wa Tanzania Yanga itaanzia Shelisheli.
Yanga itaanzia nyumbani ikiwakaribisha St Louis ya Shelisheli ikiwa ni ratiba kama ya msimu uliopita wakianzia kisiwa cha Comoro.