VIDEO: Sheikh Kipozeo, Zamaradi ndani ya Wasafi TV

Sheikh Kipozeo, Zamaradi ndani ya Wasafi TV

Muktasari:

Mkurugenzi wa Wasafi TV ambaye pia ni mwanamuziki Bongo Fleva,  Naseeb Abdul 'Diamond Plutnumz' amesema kipindi hicho ni maalumu kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Dar es Salaam: Wasafi TV jana Jumapili wamezindua kipindi maalumu kinachoitwa 'Nyumba ya Imani' katika ofisi zao zilizopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Wasafi TV ambaye pia ni mwanamuziki Bongo Fleva,  Naseeb Abdul 'Diamond Plutnumz' amesema kipindi hicho ni maalumu kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Aidha amesema, kipindi cha 'Nyumba ya Imani' kinaandaliwa na Mtangazaji Zamaradi Mketema na kinaongozwa na kusimamiwa na Sheikh maarufu, Hilal Kipozeo ambaye atakuwa akitoa mawaidha pamoja na mafundisho ya namna ya kuishi ndani ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
"Wasafi TV tumeona mwezi huu wa Ramadhani tuwaletee zawadi ya kipindi maalumu cha mafunzo namna ya kuishi kipindi hiki cha mwezi mtukufu, pamoja na kuwapa mawaidha, huku tukiendelea kujipanga zaidi," alisema Diamond.
"Nyumba ya Imani kitakuwa kinaongozwa na sheikh mahiri sana, Sheikh Kipozeo na mtayarishaji wa kipindi hiko ni Mtangazaji Zamaradi Mketema."
Ameongeza dhamira ya kipindi hicho ni kukuza imani za waumini wa pande zote za dini na ametumia wanazuoni mashuhuri na wanaopendwa hata na rika lote kama sheikh Kipozeo ambaye mbali na kuwapa ujumbe pia watu watafurahi maongezi yake kupitia kipindi hicho.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali maarufu kama, Dr Mwaka, Haji Manara, Mrisho Mpoto, Wema Sepetu, Hamisa Mobetto, Ben Pol, Dr Cheni, Steve Nyerere, Shamsa Food, Hamornize, Billnas, Khadija Kopa na wengine.