Shabiki afia uwanjani mechi ya Bournemouth kwa kuugua ghafla

Muktasari:

Shabiki huyo alikutwa na mauti wakati wa kipindi cha pili mechi ikiendelea kwenye Uwanja wa Fratton Park kutokana na watu wa huduma ya kwanza kuchelewa kumsaidia.

Klabu ya Portsmouth imethibitisha kwamba mmoja kati ya mashabiki wake amefariki uwanjani wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Bournemouth jana Jumamosi.

Shabiki huyo alikutwa na mauti wakati wa kipindi cha pili mechi ikiendelea kwenye Uwanja wa Fratton Park kutokana na watu wa huduma ya kwanza kuchelewa kumsaidia.

Taarifa ya klabu hiyo ilieleza kwamba imehuzunishwa na kifo cha shabiki wao kilichotokea wakati mechi ikiendelea uwanjani.