Shabiki Man City apagawisha

Muktasari:

Mtoto huyo amejijengea umarufuu kwa kuchambua soka

London, England. Shabiki wa Manchester City mwenye umri wa miaka 7, Braydon Bent ametokea kujizolea umaarufu mkubwa katika siku za hivi karibuni kutokana na uwezo wake wa kuchambua soka hasa mechi zinazohusu timu hiyo.

Braydon aliyezaliwa mwaka 2010 amekuwa gumzo kwa mashabiki wa soka duniani ambao wamekuwa wakifuatilia uchambuzi wake ambao amekuwa akiutoa kabla na baada ya mechi za Manchester City.

Mtoto huyo ambaye amekuwa akihudhuria mechi za City mara kwa mara katika mashindano wanayoshiriki, jina lake lilianza kupata chati pale alipochambua kiufasaha na kutabiri matokeo ya mechi baina ya Manchester City na Arsenal katika Ligi Kuu ya Uingereza ambapo aliitabiria timu yake kuibuka na ushindi wa mabao matatu ambayo baadaye yakaja kufungwa.

Miongoni mwa video zilizozua gumzo ni ile inayomuonyesha mtoto huyo akipewa lifti na kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ambapo kila mmoja alionekana kushangazwa na kumuona mwenzake.

Matukio  na idadi kubwa ya video za mtoto huyo zimewekwa katika ukurasa wa Instagram uitwao braydonbenfans ambao umeanza kutembelewa na idadi kubwa ya mashabiki wa soka duniani