Serengeti Boys imejipanga tayari

MICHUANO ya kufuzu fainali za Afrika U-17 kwa ukanda wa CECAFA itafanyika hapa nchini timu shiriki zimeanza kuwasili.

Timu zote kutoka ukanda huu wa CECAFA mara baada ya kuwasili watafanyiwa vipimo vya afya na vile vya kubaini umri kamili ambao wanatakiwa kucheza mashindano hayo.

Vipimo hivyo vinafanyika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika taasisi ya mifupa (MOI) ambapo kila mchezaji wa timu husika ambaye atacheza mashindano hayo lazima afike na kupimwa.

Mashindano yanatarajia kuanza Jumamosi ya Agosti 11-26 ambapo yatamalizika na yatafanyika katika viwanja vya Taifa, Azam Complex na Uhuru.

Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Clifford Ndimbo alisema wachezaji wote wa Serengeti Boys wamefanyiwa vipimo vyote na hakuna aliyebainika kuwa na shida yoyote kiafya na kilichokuwa mbele ni kuendelea na maandazi ya kutosha.

“Timu ipo kambini na inafanya mazoezi katika uwanja wa Azam Complex, tunamatumaini makubwa kwamba itafanya vizuri katika mashindano hayo,” alisema Ndimbo.