Samatta kuwafuta machozi Watanzania kwa kuivaa Everton

Muktasari:

  • Everton aliyokuwa icheze na Simba au Yanga, lakini baada ya kufanya vibaya katika mashindano ya SportPesa ambayo Gor Mahia ilibuka bingwa  na kupata tiketi ya kucheza na miamba hiyo ya England kwenye Uwanja wa Taifa.

 Mshambuliaji Mbwana Samatta atabeba jukumu lingine la kuiwakilisha Tanzania wakati atakapoingoza KRC Genk kuivaa Everton mwezi ujao.

Everton aliyokuwa icheze na Simba au Yanga, lakini baada ya kufanya vibaya katika mashindano ya SportPesa ambayo Gor Mahia ilibuka bingwa  na kupata tiketi ya kucheza na miamba hiyo ya England kwenye Uwanja wa Taifa.

Baada ya mechi hiyo Everton imepanga kucheza mechi ya kirafiki na KRC Genk ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake kujiandaa na Ligi Kuu England pamoja na Europa Ligi msimu ujao.

Samatta na Genk yake, watakwaana na Everton, Julai 22 mjini Genk, ikiwa ni siku tisa tu baada ya timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza kucheza na Gor Mahia kwenye uwanja wa Taifa jijini, Julai 13.

Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa Samatta kucheza dhidi ya timu inayoshiriki Ligi Kuu England.

Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano hayo, Everton itaanza rasmi kambi ya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao mwanzoni mwa mwezi Julai kabla ya kuja nchini kukwaana na Gor Mahia ambapo baada ya mchezo huo, itaenda Uholanzi itakapocheza mechi ya kirafiki na FC Twente, Julai 19 kabla ya kumalizia na Genk, Julai 22.

Timu hiyo ya Everton inatarajiwa kucheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki dhidi ya Sevilla, Agosti 6 kabla ya kuingia kwenye mikiki ya Ligi Kuu ya Uingereza ambapo watafungua dimba dhidi ya Stoke City, Agosti 12.