Samatta amva Rooney leo

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samata anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji  leo Jumamosi atakuwa katika vita ya kibabe na staa wa Everton, Wayne Rooney.

Samatta ni mshambuliaji tegemeo wa Genk wakati Rooney ni tegemeo wa Everton na leo watakutana katika mchezo wa kirafiki, ikiwa ni wiki moja na nusu tu tangu vigogo hao wa Ligi Kuu ya England walipoondoka Tanzania.

Samatta ambaye kwa sasa anavalia jezi namba 10, badala ya namba 77, ameendelea kuonyesha makeke yake katika klabu hiyo hasa baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Lommel United.

Hii itakuwa nafasi ya Samatta kujitangaza zaidi huko Ulaya baada ya msimu uliopita kufanya vizuri na timu yake ya Genk ambayo ilifika hatua ya robo fainali  ya Ligi ya Europa.