Mido ampeleka Salah kwa Real Madrid

Muktasari:

Mido ametoa kauli hiyo kutokana na kiwango cha hali ya juu kinachoonyeshwa na Salah katika Ligi Kuu England msimu huu.

London, England. Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah anaweza kuichezea Real Madrid kwa mujibu wa mshambuliaji wa zamani wa Misri, Mido.
Mido ametoa kauli hiyo kutokana na kiwango cha hali ya juu kinachoonyeshwa na Salah katika Ligi Kuu England msimu huu.
Salah amekuwa mmoja wa washambuliaji hatari England tangu alipojiunga na Liverpool akitokea Roma na sasa Mido anaamini yuko mbioni kwenda kucheza La Liga hasa katika klabu ya Bernabeu club.
"Sidhani kama Salah atakaa Liverpool kwa muda mrefu. Hivi karibuni atajiunga na Real Madrid. Hala Madrid!" Mido aliandika katika akaunti yake ya Twitter.
Salah amefunga mabao 14 katika mechi18 alizocheza Liverpool huku mabao yake sita yakitokea Ligi ya Mabingwa.