Salah mchezaji bora England

Muktasari:

  • Salah anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Misri kutwaa tuzo hiyo baada ya kucheza kwa kiwango bora Liverpool akifunga mabao 41 msimu huu.

London, England. Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu England baada ya kumpiku Kevin de Bruyne.

Salah anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Misri kutwaa tuzo hiyo baada ya kucheza kwa kiwango bora Liverpool akifunga mabao 41 msimu huu.

Mshambuliaji huyo amempiku mpinzani wake mkubwa De Bruyne wa Manchester City. Mara ya mwisho mchezaji wa Liverpool kutwaa tuzo hiyo alikuwa Luis Suarez mwaka 2014.

Tuzo ya mchezaji bora chipukizi ilichukuliwa na Leroy Sane wa Man City ambaye amechangia mafanikio ya klabu hiyo msimu huu imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Salah, alisema ni fahari kwake Liverpool na Misri kutwaa tuzo hiyo na aliahidi kuendeleza makali katika kufunga mabao licha ya kupata mafanikio hayo.