Safu ya ulinzi wa Yanga isipobadilika watajuta kwa Simba

Pemba. Yanga imetakiwa kuwa makini na safu yao ya ulinzi inayoonekana kutokuwa sawa wakiambiwa endapo wasipofanya hivyo  watajikuta katika mazingira ya mbele ya Simba.

Kauli hiyo imetolewa na kocha Mzee Abdallah  mwenye leseni B ya ukocha wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ameiambia MCL Digitala kuwa Yanga wana kikosi imara ili ubora wao mkubwa upo katika safu ya kiungo  na ushambuliaji.

Abdallah amesema kocha wa Yanga, George Lwandamina endapo anataka kuifunga Simba anatakiwa kuhakikisha anaisuka vyema safu yake ya ulinzi ambayo imeiona bado ina mapungufu kiasi ambayo yanaweza kuwaghalimu endapo watakutana na Simba wakiwa hivyo.

Alisema endapo mabeki hao wa Yanga kwa  mtindo wanaocheza wakakutana na  washambuliaji na viungo wenye mbio wanaweza  kujikuta wakifanya makosa makubwa yanaweza  kuwaghalimu ambapo wakirekebisha hilo kila kitu  kwao kiakuwa rahisi Agosti 23.

"Nimepoteza dhidi ya Yanga matokeo  nimeyakubali, tulijiandaa vyea kuwazuia, lakini  niseme wenzetu walikuwa bora zaidi yetu wameonyesha kwamba wako sawa najua kwamba wanajiandaa na ligi na kucheza dhidi ya Simba,"alisema Abdallah

"Tofauti na nilivyokuwa nawajua jana tumeona Yanga wakibadilika katika mbinu wakicheza soka la kwenda mbele zaidi wasiwasi wangu ni safu yao ya ulinzi naona bado haijawa katika kiwango bora kuna kazi kocha wao anatakiwa  kuifanya wakikutana na timu yenye wasambuliaji wenye kasi wanaweza kupata shida.